![]() |
| Maafisa wa elimu wakiongozwa na mawaziri Matiang'i, Nkaisary na Mucheru. |
Robert mwangi.
Waziri
wa elimu humu nchini Fred Matiang’i ametoa onyo kali kwa mtu yeyote aliye na
mpango wa kuhitilafiana na mitihani ya KCPE na KCSE itakayo fanyika kuanzia
mwezi mwezi ujao.
Matiang’i vilevile
amewaonya wakenya walio na mpango wa kusaidi
wanafunzi katika wizi wa mitihani hiyo akisema kuwa watakabiliwa vikali
kisheria.
Waziri huyo akiwa pamoja na waziri wa usalama wa ndani
Joseph Nkaisery, na mwenzake wa habari, teknolojia ya mawasiliano Joe Mucheru, wameafikiana kuwa usalama wa karatasi za
mitihani mwaka huu utakuwa wa hali ya juu.
Mtihani wa KCPE utaanza Jumanne tarehe mosi mwezi Novemba huku mtihani wa KCSE ukitarajiwa kuanza jumatatu ya wiki
itakayo fuata.

No comments:
Post a Comment