Ambwene Yesaya al maarufu kama AY ameungana na mkali wa bongo flava Diamond Platnumz kufanya remix ya hit ya ZIGO na tayari wanashoot video afrika kusini.
![]() | |
AY (kushoto) na Diamond |
Habari hizi
zilitolewa jana na kampuni ambayo inatengeza video ya AY, Studio Space Pictures ya afrika kusini.
Studio hii
ilitupia picha kwenye mtandao wa Instagram na kuandika “earlier today with @aytanzania @diamondplatnumz #ZigoRemix #StudioSpacePictures “
Haijabainika
kama ni Diamond pekee ambaye ameshirikishwa lakini huenda mastaa wengine pia
wakahusishwa na msanii AY.
AY kwa sasa
anavuma na ngoma aliyoshirikishwa na mtoto wa kike kutoka hapa Kenya Avril Nyambura, No Stress.
Sio mara ya
kwanza kwa AY na Diamond kukutana kwani Diamond ashawahi kutupia mistari katika
ngoma ya AY iliyoitwa Asante. #Asante
No comments:
Post a Comment