Thursday, 17 December 2015

ZAIDI YA FAMILIA MIA MOJA KUSALIA BILA MAKAO, KWALE.

NA JULIUS KARIITHI
Athari ya mafuriko, Lunga Lunga, Kaunti ya Kwale, kama ambavyo
ilisababishwa na mvua kubwa ya El Nino.


Watu wengi wamefariki, mali ya dhamana yameharibika, na boma nyingi zimesalia mahame kufuatia    fujo ya mvua inayoendelea ya Elnino ,ambayo yatabirika kuwa yaweza chukua muda mrefu kusimama.
Tunapozungumza zaidi ya familia 100 kutoka eneo la Vanga, huko Lunga lunga, kaunti ya Kwale zimesalia kuwa bila makao, vile vile mazao pamoja na mifugo yao haikusazwa na wingi na msukumo mkubwa wa maji, kwani ilisombwa  Kufuatia mafuriko ya mto wa Maumba.
Kwa maneno yake Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kutoka Vanga, Mohamed Ferunzi , vitongoji vya Dziriphe,Kiwegu Chuini ni baadhi ya maeneo yaliothirika zaidi na mafuriko hayo.
Mwanaharakati huyo aidha ameeleza hofu ya kuangamia kwa mali zaidi iwapo suluhu ya haraka haitapatikana hususan kuzuia majanga yanayotabiriwa, kwani kwa Sasa taifa la Tanzania linashuhudia mvua inayotabiriwa kuendelea kwa muda wa miaezi sita ijayo.
Baadhi ya mambo yanayonuiwa kuadhiri wakenya iwapo mvua hii itaendelea, ni pamoja na matatizo ya usafiri, kwani wakati wa mvua washika dau katika sekta ya usafiri hapa nchini huchukua mwanya huu kuwanyanyasa wasafiri kwa kupandisha nauli kwa pakubwa, hivyo kufanya kuwa mzigo mkubwa kwa wengi haswa kwa wanaotumia teksi na pikipiki.




No comments: