Wenyeji wa kijiji cha Enyapora Mumias, Kakamega county wamepigwa na butwaa baada ya
jeneza kulipuka na maiti kuwaka moto.
![]() | |
Jeneza la Mfu |
Kitendo hiki cha kushangaza kilitokea wikendi iliyopita
ambapo walikuwa wanajitayarisha kuzika maiti hiyo.
Maiti hiyo ni ya mwanamke wa umri wa makamo ambako
walioshuhudia kisa hicho walisema kuwa maiti ilichomeka miguu na pia sehemu ya
ndani ya jeneza.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa hajafurahishwa na
mumewe baada ya mume huyo kutomjengea
nyumba licha ya kumzalia watoto.
Kulingana na mwenyeji wa humo, mwanaume katika jamii ya
waluhya ni sharti amjengee nyumba nzuri mkewe ili kumridhisha lakini bwana wa
mke huyu hakuwa ametekeleza hilo.
No comments:
Post a Comment