Wednesday, 16 December 2015

MBUNGE MWINGINE TENA KULALAMIKIA HADHI YA CHAKULA MBUNGENI

By Elvis Owuor

Mbunge wa eneo la Sirisia mheshimiwa John Waluke amegonga vichwa vya habari kwa kutoa malalamishi ya vyakula wanavyopewa kule bungeni kuwa haviwaridhishi kamwe hususan chumvi na maziwa ni adimu kwa chakula na chai mtawaliwa.
Mheshimiwa Waluke alionekana mbele ya kamera ya video hapo jana akinoa makali yake akiwa mahali pa kupokea maamkuli na kikombe cha chai na birika kisha akaelezea wanahabari haya “too broke to buy milk and was now serving black tea.”
“Parliament cannot afford a packet of milk that costs Sh50, this is bad… hii kabirika ni Sh100 with no milk… hakuna hata chumvi kwa mboga. Nothing!”Mbunge huyo alifoka.

Mh Waluke hapo awali ameorodheshwa wa pili kwa utendakazi ambapo ulionyesha wabunge wa Nairobi kuwa na utendakazi duni.
matokeo haya yalitolewa na shirika la Infotrak Research & Consulting.Wakati utafiti ulijumulisha watu 29,000 waliohojiwa hapa nchini anga watu mia moja moja kutoka kwa kaunti ndogo mnamo desemba mwaka jana(2014) na Februari mwaka(2015) huu .
maswali yaliyoulizwa ilihusu utendakazi wa wabunge wao.



No comments: