![]() |
Gavana wa Bomet Isacc Ruto |
Ben Kirui
Gavana wa
Bomet Isaac Ruto amepinga hafla ya maombi ambayo imepangwa na rais Uhuru
Kenyatta na Naibu wake William Ruto itakayoandaliwa katika uwanja wa Afraha
mjini Nakuru jumamosi ijayo.
Mkutano huo wa maombi ambao Rais
Kenyatta alitangaza pindi tu mahakama ya ICC ilipotupilia mbali kesi iliyokuwa
ikimkabili Naibu Rais na Mwanahabari Joshua arap Sang’ umetajwa na Gavana Ruto
kama wa kukejeli waathiriwa wa ghasia za 2007.
Gavana Ruto badala yake amewataka rais Kenyatta na naibu wake Ruto
wawazie kuhusu vile wataunganisha taifa hili na kuliponya kabisa kutokana na
athari za muda mrefu za ukabila na misukosuko ya kijamii.
No comments:
Post a Comment