![]() |
Wanawake watano na mvulana mmoja walifariki huku 59 wakijeruhiwa kwenye ajali ya usiku wa kuamkia leo. |
Ben Kirui
Watu watano
wamefariki huku wengine 59 wakikwepa na majeraha baada ya basi moja kupoteza
mwelekeo na kuanguka katika eneo la Ngele Mbooni mashariki kaunti ya Makueni katika
barabara kuu ya kutoka Mjini Tawa kuelekea Macii.
Kulingana na
OCPD wa Mbooni mashariki James Baraza watatu walifariki papo hapo huku wengine wawili
wakifariki wakati wakikimbizwa hospitalini.
Miongoni mwa
waliofariki katika ajali hiyo ya usiku wa kuamkia ni wanawake wanne na mvulana
mmoja wa miaka 7.
59
waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Tawaa na wengine katika
hospitali ya Makueni level 4.
Baraza
amesema huenda basi hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi.
No comments:
Post a Comment