Friday, 18 November 2016

NI MARUFUKU KWA NYOTA WA UINGEREZA KUHUDHURIA SHEREHE ZA USIKU

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza, 'the three lions'

KAPEDO JNR
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wamepigwa marufuku dhidi ya kuhudhuria sherehe za usiku, wakiwa katika ziara yao ya kimataifa

Shirikisho la kandanda nchini Uingereza FA, linachunguza madai kwamba wachezaji kadha walikua nje ya kambi hadi saa za usiku wa manane, siku ya Jumamosi baada ya mechi yao dhidi ya Scotland, mechi ambayo Uingereeza ilishinda kwa mabao matatu bila jibu

Hii inakuja siku 3 baada ya Uingereza kuandikisha sare ya kufungana mabao 2 dhidi ya Uhispania kwenye mechi ya kirafiki iliyogaragazwa katika uwanja wa Wembley


Nahodha wa Uingereza muite Wayne Rooney Warza aliomba msamaha baada ya picha zilizooneshana akiwa mlevi katika harusi moja usiku huo, kitendo ambacho kilimgadhabisha mkufunzi wa timu ya Manchester United Jose Mourinho

No comments: