Sunday, 11 December 2016

WALINZI WA RAIS MIONGONI MWA WALIOANGAMIA KWENYE AJALI NAIVASHA

Mabaki ya magari yaliyoteketea wakati lori lilipuka

Ben Kirui

Maafisa 11 wa kitengo cha GSU ni miongoni mwa watu 33 waliofariki Jumamosi usiku kwenye barabara kuu ya Naivasha-Nakuru wakati lori lililokuwa limebeba bidhaa zinazoshika moto kugonga matuta barabarani na kupoteza mwelekeo, kisha kugonga magari mengine na kushika moto.

Kwenye taarifa kutoka Ikulu ya Nairobi msemaji wa ikulu Manoa Esipisu amesema kuwa Maafisa hao kutoka kwa kitengo cha Ulinzi wa Rais walikuwa wanasafiri kutoka kaunti ya Bomet ambapo Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walikuwa wamezuru mapema jana.

Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa rambirambi kwa familia za wahanga.

No comments: