Thursday, 5 January 2017

WATU WATATU ZAIDI WAFARIKI KUTOKANA NA AJALI NYAKACH

Mabaki ya matatu iliyohusika katika ajali hiyo ya mapema leo.

Ben Kirui

Idadi ya watu waliofariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya Katito-Pap Onditi imeongezeka na kufikia 14.

Hii ni baada ya watu watatu zaidi waliokuwa wakipokea matibabu katika hospitali ya Nyabondo mjini Kisumu kufariki.

Manusura wengine wanne wanaendelea kupokea matibabu katika kituo hicho ambapo walikimbizwa baada ya ajali hiyo ya mapema leo asubuhi.

Kwa mujibu wa kamanda wa trafiki mkoani Nyanza, Andres
Naibei, ajali hiyo ilitokea katika eneo la Daima wakati dereva wa matatu kukosa udhibiti na kutumbukia katika mtaro ikiangamiza abiria 11 papo hapo.

Naibei anasema baadhi ya waathirika walikuwa wanafunzi waliokuwa wakisafiri kurejea shuleni


Matatu hiyo ilikuwa ikielekea Kisumu kutoka Sirare kaunti ya Migori 

No comments: