Wednesday, 29 April 2015
MATHARE YAPATA UFADHILI WA BRITAM
Na Moses Ngige
Timu ya MATHARE united inayoshiriki ligi kuu nchini imetia mkataba wa
miaka mitatu ya udhamini na kampuni ya BRITAM.
Udhamini huo wa shilingi milioni sabini na tano [75,000,000/] umezinduliwa Leo Jumatano
katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.
Daktari Benson Wairegi, mkurugenzi mkuu wa Britam, ameahidi kuwa ikiwa
timu hiyoitajizolea matokeo ya kuridhisha katika ligi, huenda wakaongeza muda wa
udhamini.
Amesema kuwa amechagua kuidhamini timu hiyo kwani yeye amelelewa
maeneo ya mathare na sasa ni wakati kuiunga jamii mkono.
Bob Munro ambaye ni mwanzilishi wa timu hiyo, ameelezea furaha yake na
kusema kuwa sasa ni wakati timu hiyo ionyeshe makali yake.
" Ufadhili wa timu hii unaonyesha kuwa kuna matumaini kutoka kwa wadhamini wetu, kuwa Mathare inao uwezo wa kufanya vyema katika ligi kuu ya humu nchini, tunashukuru sana ufadhili wa Kampuni ya BRITAM na tunaihakikishia kampuni fadhili kuwa tutajikakamua tuwezavyo kufanya vyema katika ligi hii na ligi nyinginezo," alisema Bw Munro.
Timu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya kumi na moja kwa alama kumi.
Mhariri wa Makala- William Khaemba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment