Tuesday, 19 May 2015

Keter na Birdi watarajiwa Kotini leo







By Rashid Mwazuma

Mbunge wa Nandi hills Alfred Keter mbunge maalum wa URP Sonia Birdi wanatarajiwa leo katika mahakama ya Naivasha kushtakiwa kwa kosa la kufanya usumbufu katika kituo cha kupima uzani malori cha giligili  yapata miezi miwili iliopita.

 Hii ni baada ya mahakama kuu kukataa kuwapa amri waliomba kuzuia kukamatwa na kushtakiwa kwao.

Katika uamuzi wake, jaji Mumbi Ngugi amesema kwamba wabunge Keter na Birdi wameshindwa kuonyesha jinsi haki zao zitakiukwa endapo watakamatwa na kushtakiwa na akaagiza washtakiwe kesho .

Kesi hiyo itatajwa tarehe 19 Juni ili maagizo zaidi yatolewe.

No comments: