Thursday, 24 December 2015

ALSHABAAB,ISIS NA ALQAEDA WATISHIA MASHAMBULIZI KRISMASI NCHINI



 NA ELVIS OWUOR

Alshabaab wakipewa amri ya mashambulizi



Wakenya wametakiwa kuwa waangalifu msimu huu Krismasi kwa minajili ya usalama wao dhidi ya kundi la wanamgambo wa alshabaab kujigawanya katika makundi mawili ili kupata ushindi katika maovu wanayotarajia kutekeleza.

Huku mbwembwe za kila aina zikionekana kwa wakenya wengi , maeneo ya burudani na masoko yakiwa yamefurika furi furi  sherehe za krismasi kuanza rasmi Taarifa inayojiri kutoka kwa idara ya usalama nchini inaelezea jinsi wanamgambo wa Alshabaab wanavyoazimia kutekeleza mashambulizi humu nchini limepokelewa kwa uangalifu mkuu na inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinet.

Boinet amesema kuwa sasa kundi la alshabaab limejigawanya kwa upande Mbili moja ikijiunga na wanamgambo wa Islamic State na lingine likiunga mkono Al-Qaeda.
Inadaiwa kundi la alshabaab linalounga mkono ISIS linafanya operesheni yake Kaunti ya Mandera huku lile liko nyuma ya Al-Qaeda limekita kambi katika msitu wa Boni ilioko eneo kusini la Kenya
Boinet adressing press


Inspekata Jenerali ameelezea kuwa makundi haya mawili yanashindana kueneza ajenda ya jihad ambayo itakuwa mbaya zaidi iwapo itatokea.

Vile vile Boinet amesema kuwa katika basi liliotekwa nyara jumatatu ya wiki hii ambapo waislamu waliweza kuwakinga wakristo waliokuwa wakisafiri nao eneo la El Wak kaunti ya Mandera lilfanywa na ISIS.

Aidha Boinet amesema kuwa genge hilo kutoka mandera linalongozwa na Isaak Osman Ali almaarufu kama Okola,, Abdifata Basre na  Mohamed Bilal huku lile ya Al-Qaeda likiongozwa na Omar Ahmed Abdumanan.

No comments: