![]() | |
|
Tukio lingine la
kustajabisha zimejitokeza katika kaunti ya Mandera ambapo maafisa wawili wa
usalama wameuwawa na wengine kujeruhiwa kufwatia mashambulizi ya kigaidi
yaliyosababishwa na kundi la wanamgambo wa Al Shabab.
Gavana wa Mandera ,Ali Ibrahim Roba,
alithibitisha mashambulizi hayo yaliyotekelezwa katika eneo la Kurkura, karibu
na lungu baina ya mpaka wa, Elwak na Laffe, na kuwauwa maafisa wawili na
kuwajeruhi wawili pia.
Ni
matukio ya kigaidi ambayo yanazidi kushuhudiwa hapa nchini wakati idara ya
polisi inazidi kubambana vikali na maswala ya kigaidi haswa katika msimu huu wa
Krismasi.
Mashambulizi
haya yanajiri siku moja tu baada ya ya kifo cha gaidi mmoja wa Alshabab,
aliyejaribu kutega vilipuzi katika kaunti hiyo ya Mandera.

No comments:
Post a Comment