![]() |
Athari ya moto kwa binadamu na mali |
Mwanamke mmoja amemteketeza mkewe kiasi cha kumuacha na majeruhi makali katika kijiji cha Nembure kaunti Embu .
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32, kwa sasa anatetea maisha yake katika hospitali ya Embu ambapo kulingana na OCPD wa eneo hilo, James Karisa, mwanamume huyo afahamikaye kama Ibrahim Muriithi awali alikuwa ametengana na mkewe na hivyo baada ya mke wake kudinda kurudiana , jamaa huyo akaamua kumteketeza.
Karisa aliongeza kuwa mwanamume huyo alimdanganya mkewe kwamba angependa wawe na mazungumzo ya kibinafsi na baada ya mke huyo kukaidi takwa lake,inanuwa kuwa alimshika mkono na kuanza kupiga vita kabla ya kummiminia petroli na kumteketeza.
Jamaa huyo wasasa amekamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi huku akisubiri kufikishwa mahakamani.

No comments:
Post a Comment