Wednesday, 30 December 2015

WATU 157 KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA WIZI WA MTIHANI

Na JULIUS KARIITHI


Afisa mkuu mtendaji wa tume ya mitihani, knec Joseph Kivilu awali

 akihutubia wanahabari

Tusisalia kwenye maswala ya elimu Afisa mkuu mtendaji wa tume ya mitihani ya kitaifa, Joseph Kivilu, amesema kuwa takriban watu 157 wamefunguliwa mashtaka kwa kujihusisha na wizi wa mitihani.
Akizungumza wakati wa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCPE hii leo, Kivilu amesema kuwa aliofungwa and kuhukumiwa kwa wizi huo wa mtihani ,ni pamoja na wakuu wa shule, manaibu wao, wanafunzi wa vyuo, wazazi, maafisa wa polisi pamoja watahiniwa wenyewe.
Kivilu hivi majuzi alisema kuwa hakutakuwa na kuorodheshwa kwa shule na mtindo wa kuyatangaza matokea utakuwa tu kama wa mwaka uliopita.
Mtihani huo wa kitaifa wa KCPE ulijumuisha takriban watahiniwa 937,467 kote nchini.



No comments: