NA ELVIS OWUOR
![]() |
| George Wainaina kupelezwa na EACC |
Alikamatwa pamoja na katibu wake kwenye jaribio la kutaka kumhonga seneta wa Nairobi Mike Sonko shilingi milioni moja pesa taslimu za Kenya ili kunyamazisha vita dhidi ya ufisadi.
Wainaina alikamatwa na wapelezi hao akitoka katika kanisa moja alipoenda kutoa mchango wake wa matanga na kufikishwa hadi makao makuu ya upelelezi chini ya ulinzi mkali.
Wainaina aidha anachunguzwa kwa madai mengi ikiwemo shamba la mamilioni ya Loresho ilioko eneo la Westland.
Shamba hilo lilikuwa linamilikiwa na mwekaji wa binafsi ambaye tayari alikuwa ameanzisha ujenzi wa kuhudumia wakaazi wa Nairobi kupokea maji safi.
Hii ni baada ya senataor sonko kuingilia kati na hata kuongoza maandamano ya amani kabala ya kumfikia rais kutoa suluhu.
Inspector jenerali wa polisi joseph Boinet aliamrisha maafisa wake pamoja na afisa mkuu mtendaji wa EACC kuchukua hatua madhubuti.
Mwekaji huyo wa kibinafsi hapo awali alikuwa amepuuzilia mbali agizo la kuendeleza ujenzi katika shamba hilo.
Hata hivyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi tu uchunguzi utakokamilika.
Gavana wa Nairobi Evans Kidero mapema hii leo aliandaa kikao kuhusu kukamatwa kwake mkuu wa wafanyikazi George Wainaina.
Unaweza ukamshirikisha mwenzako pia kwenye keja ya FB,Twitter ama IG

No comments:
Post a Comment