Thursday, 7 January 2016

MUME AMDUNGA MKEWE KISU, KWA NINI?....



Na KakaMusa
Picha kwa hisani ya The Star.

Mwanaume amdunga mkewe kwa kutumia kisu kwenye shavu na kumuumiza mfupa baada ya mzozano wa kifamilia huko Khorof Harar, Kaunti ya Wajir.
Fatuma Ibrahim yungali na kisu shavuni mwake kwani daktari walidai kuwa hawangeweza kukitoa kisu hicho kwa ugumu wa kuhatalisha maisha ya mwanamke huyo wa miaka 32.
Ibrahim ambaye ni mama wa watoto wanne atasafirishwa Nairobi kwa upasuaji katika hospitali kuu ya Kenyatta.
Wanawake walijitokeza kwa wingi kuumpa nguvu Ibrahim na kuikashifu serikali kwa kudhalilisha haki zao.
“Haki za wanawake ni sharti zizingatiwe ili kuzuia mashambulizi na dhuruma za kijinsia,” alisikikia akisema mwanamke Sahara Keynan.
Hata hivyo, OCPD wa Wajir, Benson Mukumbi alisema kuwa Mohamed Deeq ambaye ndiye kutekeleza unyama huo tayari ametiwa mbaroni na atafikishwa mahakamani siku ya ijumaa. #ASANTE

No comments: