Friday, 29 January 2016

RAILA ALALAMIKIA HATUA YA KPA KUFUNGA SHEHENA INAYOMILIKIWA NA JOHO


Kiongozi wa upinzani Raila Odinga

 Ben Kirui

KIONGOZI wa CORD Raila Odinga ameisuta serikali kwa kuamuru mamlaka ya ukusanyaji ushuru KPA kufunga vituo viwili vya kuhifadhi shehena vinavyomilikiwa na familia ya gavana wa mombasa Ali Hassan Joho.
Kwenye taarifa aliyotuma kwa vyombo vya habari Odinga amesema hatua hiyo ni mpango wa serikali ya Jubilee kutisha na kuhangaisha magavana wa upinzani.
Baadhi ya wabunge wa mrengo wa Cord wakiongozwa na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir nao wamelalamikia hatua hiyo wakisema imechochewa na mahasimu wa Joho.
Kwenye waraka mkurugenzi mkuu wa KPA Gichiri Ndua anasema shughuli katika vituo hivyo imesistishwa kwa muda usiojulikana.
Vituo hivyo ni miongoni mwa vingine vinavyochunguzwa kwani vimehusishwa na wafanyibiashara walaghai wanaoingiza nchini bidhaa za magendo na hata kukwepa kulipa ushuru.

No comments: