Friday, 12 February 2016

RUFAA YA JAJI PHILIP TUNOI YACHUKUA MKONDO MPYA


Jaji Philip Tunoi na wakili wake Pheroze Nowrojee

 BEN KIRUI
RUFAA ya kuamua umri wa kustaafu kwa Jaji Philip Tunoi wa Mahakama ya Juu hii leo imechukua mwelekeo mpya baada ya ombi la kujiondoa kwa mmoja wa majaji saba aliyehukumiwa na Tunoi miaka 22 iliyopita.

Jaji GBM Kariuki amekiri kwamba aliadhibiwa na Jaji Tunoi aliyekuwa miongoni mwa majaji wa Mahakama ya Rufaa waliompata na hatia ya kuidharau mahakama. Jaji Tunoi anapinga uamuzi wa majaji watano wa mahakama kuu waliomwamuru astaafu wakidai amehitimu umri wa kustaafu.
Hayo yakijiri wanahabari na umma kwa jumla walifungiwa nje ya mahakama ya juu wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo baada ya mawakili wa Tunoi kuiomba mahakama kuendesha vikao vyake faraghani.

Jopo la majaji 7 linasikiza kesi hiyo ya jaji Tunoi ambaye anapinga sheria inayomtaka kustaafu baada ya kutimu miaka 70. Rufaa ya jaji Tunoi inawadia wakati ambapo rais Uhuru Kenyatta anasubiri kupokezwa ripoti inayopendekeza kubuniwa jopo maalum la kumchunguza Tunoi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi millioni 200 kutoka kwa gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero.

No comments: