Monday, 15 February 2016

MPINZANI MKUU WA MUSEVENI AKAMATWA





Mgombea wa urais Kizza Besigye



Ben Kirui.
Mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi mjini Kampala.

Gari lake lilikuwa likipitia barabara ya Jinja, mjini Kampala, msafara wake ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, pale polisi walipotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.
Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi lakini akaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.

Polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza uchukuzi mjini.
Besigye alipangiwa kufanya mikutano ya kampeni katika mji mkuu wa Kampala.

No comments: