![]() |
| Rais Kenyatta wakati wa hafla ya kufuzu kwa askari jela |
Rais amesema hatua hiyo itazuia wafungwa hao kutoeneza itikadi hizo kwa wafungwa wengine.
Kwa sasa ni wafungwa waliohukumiwa kunyongwa pekee ndio hutengwa na wafungwa wengine gerezani nchini.
Akihutubu wakati wa hafla ya kufuzu kwa zaidi ya askari jela 2,000 Rais Kenyatta ametangaza mpango huo huku Akisema serikali yake imeanzisha mpango wa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikikabili idara ya magereza.
Kenya
imekabiliwa na tishio la wahalifu wenye itikadi kali, hasa kutoka kwa kundi la
Kiislamu la al-Shabab kutoka Somalia

No comments:
Post a Comment