Monday, 22 February 2016

WAIGURU AFIKA MBELE YA EACC


Aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Ann Waiguru

 Ben Kirui
Aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru amefika mbele ya tume ya maadili na ufisadi asubuhi leo huku mfanyibiashara Josphine Kabura akitarajiwa kufika mbele ya EACC hiyo kesho.
Waiguru ametajwa kama mhusika mkuu wa sakata ya ufujaji wa shilingi milioni 791 za shirika la huduma kwa vijana NYS
Kufika kwa Waiguru EACC kunatokana na hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani na mfanyibiashara Josephine Kabura ambaye anasema alishirikiana na Waiguru kutekeleza ufujaji huo.

No comments: