![]() |
| Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye akikamtwa nyumbani kwake |
Ben Kirui
Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye
kwa mara nyingine ameripotiwa kukamatwa kutoka nyumbani kwake eneo la Kasangati
nchini Uganda.
Katika kisa
hicho wanahabari wawili pia wamejeruhiwa baada ya kunyunyuziwa piliipili
machoni na polisi waliokuja kumkamata kiongozi huyo.
Besigye amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake. Afisa wa chama cha FDC amefichua kwamba Besigye amekuwa akizuiliwa ili asikusanye ushahidi wa kupinga matokeo ya uchaguzi ambao ulikamilka siku ya alhamisi. Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais.

No comments:
Post a Comment