![]() |
| Waziri Matiang'i na wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Keveye |
Pharence Nduko
Waziri wa elimu Dkt.Fred Matiang'i amewataka walimu wakuu
kutoa vyeti vya wanafunzi.
Wakurugenzi wa elimu wamepewa muda
hadi mwishoni mwa mwezi kuwasilisha orodha ya shule ambazo zinashikilia hati za
kukamilisha shule za wanafunzi.
Aidha, Matiangi amewasuta wakuu
wa shule ambao bado wanashikilia hati hizo kwa dai la masalio ya karo. Anasema
hatua hiyo imewanyima wengi wa vijana kuendelea na masomo. Ametoa onyo kali
dhidi ya wakuu watakaoendelea na tabia hiyo.

No comments:
Post a Comment