Saturday, 27 February 2016

JE, RUTO ATAWEZA KUTHIBITI MAKALI YAKE KISISASA KATIKA BONDE LA UFA?


Naibu rais William Ruto na mgombea useneta Kericho Aaron Cheruiyot

 Ben Kirui

Joto la kisisasa linazidi kupanda huku zikisalia siku za kuhesabu kabla ya wenyeji wa kaunti ya kericho kuelekea kwenye debe kuamua mbivu na mbichi kwenye kinyang’anyiro cha useneta.
Naibu wa rais William Ruto amepiga kambi kule kericho kumpigia debe Aaron Cheruiyot atakayepeperusha bendera ya muungano wa Jubilee.
Cheruiyot anakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa Paul sang wa Kanu anayepigiwa debe na waasi wa URP wakiongozwa na gavana wa Bomet Isacc Ruto.
Uchaguzi mdogo wa useneta Kericho umepigiwa upato kama kitambulisho cha hali itakavyokuwa mwaka ujao huku macho yote yakielekezwa kwa Naibu wa Rais kubaini atakavyokabiliana na waasi wanaolenga kupunguza makali yake kisiasa.



No comments: