Wednesday, 3 February 2016

WAMILIKI WA TEKSI WATISHIA KUGOMA


Huduma ya teksi ya Uber


Ben Kirui

Wamiliki wa magari ya teksi hapa jijini Nairobi wanatishia kugoma ili kuishinikiza serikali kuipiga marufuku huduma ya teksi ya Uber. Msemaji wao Mwangi Mubia amesema kwamba hawana njia nyengine ya kusuluhisha mgongano kati yao na wenye magari wanaotumia huduma hiyo ya mtandao wa Uber.' Aidha wamiliki hao wamekariri kuwa ni wao ambao wanastahili kulalamika kwani mbinu zinazotumiwa na wahudumu wa uber zinawanyima njia ya kujipa riziki.
Hayo yanajiri wakati ambao serikali inajiandaa kuwafikisha mahakamani madereva wawili wa teksi waliokamatwa kwa madai ya kuwashambulia wapinzani wao wanaotumia huduma ya Uber.  

No comments: