Thursday, 10 March 2016

BAYERN TAYARI KUMTEMA STAA MARIO GOTZE.


Nyota wa Bayern Munich Mario Gotze.

Mwangi K. Githinji

Klabu cha Bayern Munich kimemwambia nyota wake Mario Gotze kuwa yuko huru kughura miamba hao.
Gotze mwenye umri wa miaka 23 anakumbukwa na  wengi hasa kutokana na goli la pekee alilofungia Ujerumani kwenye kombe la dunia la mwaka 2014, lilowapa ubingwa wa taji hilo.
Wakurugenzi wa Bayern wamedinda kumpa mkataba mpya kwani inaaminika kuwa hayuko katika mipango ya kocha Carlo Ancelotti, anayetarajiwa kuchukua hatamu mwishoni mwa msimu huu.
Tayari vilabu kadhaa vimejitokeza vikiwania sahihi yake, ikiwamo miamba wa Italia Juventus,Liverpool na Manchester United vya uingereza.
Liverpool wanaongoza katika mbio za kumwania Gotze kwa kuwa mkufunzi wao  Jurgen Klopp ndiye alimuibua kutoka kwa timu ya makinda ya Borussia Dortmund alipokuwa kocha wa mibabe hao.
Kwenye taarifa zingine ni kuwa mlinzi wa Bayern Munich Medhi Benatia amepuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kuondoka Bayern msimu huu utakapomalizika.
Benatia anayechezea timu ya taifa ya Morocco alijiunga na Bayern kutoka Roma mnamo Agosti mwaka 2014, lakini majeraha yamemnyima nafasi ya kung’aa katika klabu hicho.
Ameeleza kuwa yeye anapania tu kusaidia timu yake kushinda taji la Bundesliga na la klabu bingwa ulaya, mbali sio jinsi atakavyohama kutoka Bayern.
Mkataba wake wa sasa na klabu hicho utamalizika Juni mwaka 2019.

No comments: