![]() |
| Gavana wa Mombasa Hassan Joho na Kinara wa Cord Raila Odinga |
Ben Kirui
Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan
Joho sasa amemwandikia waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery akitaka
rufaa dhidi ya agizo la kuregesha bunduki alizonazo.
Kupitia wakili
wake Ahmed Nassir Abdullahi, Joho amemshutumu msimamizi wa utoaji wa leseni za
bunduki Samuel Kimaru akisema maagizo hayo yalitolewa kwa misingi ya kisiasa.
Joho pia
anadai Kimaru alitoa agizo hilo kufuatia uchaguzi mdogo wa Malindi ambapo ODM waliwashinda
Jubilee na kuitaja hatua hiyo kama kinyume cha sheria.
Wakati huo huo Kamanda
mkuu wa polisi kanda ya Pwani Francis Wanjohi amekanusha uvumi unaoenea kwamba
waliokuwa walinzi wa gavana wa Joho wamekamatwa na kuzuiliwa
katika kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa.

No comments:
Post a Comment