CHIFU WASHAMBULIWA NAKURU.
 |
| Pombe haramu. |
Chifu mmoja anauguza majeraha katika hospitali ya
Nakuru level 5 baada ya kudungwa mkuki mguuni wakati alikuwa akiendesha kampeni dhidi ya pombe haramu huko
Lower Solai kaunti ya Nakuru.
Samuel Totona wa kata ya maji tamu akiandamana
na machifu wenzake walishambuliwa na kundi la vijana baada ya kumkamata
mshukiwa wa biashara ya pombe haramu katika eneo la Arusto.
Chifu huyu amelaumu maafisa wa utawala eneo hilo kwa
kutohakikisha kuwa washukiwa wanashtakiwa na kumaliza biashara ya pombe
haramu.
No comments:
Post a Comment