By Lena Juliet.
Walimu watakaopatikana wakiwaadhibu wanafunzi kinyume na sheria
watachukuliwa hatua.
Wizara ya elimu
kupitia mkurugenzi wa masuala ya ubora wa elimu Pius Mutisya anasema
wanaendelea kupokea ripoti kuhusu kuadhibiwa kwa wanafunzi licha ya adhabu hiyo
kupigwa marufuku.
Anasema wizara ya elimu haitasita kuwachukuliwa
hatua za kinidhamu walimu wanaowaadhibu watoto kwa kutumia kiboko na kuwa
huenda wakaachishwa kazi.
Anasema walimu hao
hawatatetetewa na serikali iwapo watafikishwa kotini. Amewataka walimu kubuni
njia nyingine za kuwaadhibu wanafunzi.

No comments:
Post a Comment