Mwangi K. Githinji.
Kiungo wa Tottenham Nabil Bentaleb atakuwa nje kwa kipindi cha wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji katika goti lake.
![]() |
| Mchezaji wa Tottenham Nabil Bentaleb. |
Kiungo huyo alipata jeraha hilo alipokuwa anachezea timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 21 waliyshindwa mabao 3-0 na Leicester japo anatarajiwa kurejea kwenye mazoezi kabla ya msimu huu kumalizika.
Bentaleb ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Algeria amechezea Tottenham mechi mbili pekee msimu huu baada ya kupata jeraha katika majira ya moto lililomuweka nje kwa miezi mitatu.
Kwingineko ni kuwa nyota wa timu ya Arsenal Mesut Ozil amepuzilia mbali madai kwamba anapanga kuondoka klabuni
hicho ikiwa Arsene Wenger ataendelea kuwafunza miamba hao wa uingereza.
Kiungo
huyo mjerumani ayesajiliwa na Wenger kutoka Real Madrid kwa ada ya yuro milioni
42.5 mnamo mwaka wa 2013 ameeleza kuwa
bado anamheshimu sana kocha huyo.
Tayari
Ozil ameshinda mataji mawili ya FA tangu
alipojiunga na Arsenal na anakaribia kuvunja rekodi iliyowekwa na Thierry Henry
ligini uingereza ya kusaidia kufungwa kwa magoli mara mengi zaidi.

No comments:
Post a Comment