Makundi ya kinamama, vijana na
walemavu kaunti ya Mombasa yanatazamiwa kufaidi na shilingi bilioni mbili
zilizotengwa na serikali kusaidia kuboresha miradi inayoendeshwa na makundi
hayo.
Kaunti ya Mombasa imetengewa
shilingi milioni arobaini na sita ambazo zimepangwa kugawanywa kwa makundi yote
yaliyosajiliwa na ambayo tayari yanaendeleza miradi mbali mbali.
Haya yamesemwa na mwenyekiti
wa makundi ya walemavu eneo bunge la changamwe James Karanja, amabaye
amesema makundi yatakayo pokea fedha hizo hayahitaji kuzilipa tena kwa
serikali, hivyo kuyahimiza makundi ya walemavu kutoogopa na kujitokeza kwa
wingi ili wafaidi na mpango huo.

No comments:
Post a Comment