Tuesday, 29 March 2016

VITUO ZAIDI VYA POLISI KUJENGWA LAMU.


kituo cha polisi

By Lena J.

Vituo tisa vya polisi vitajengwa katika maeneo tofauti kaunti ya Lamu ili kuimarisha usalama na kurejesha utulivu kutokana na mashambulizi ya kila mara kutoka kwa waasi wa alshabaab.

Haya ni kwa mujibu wa James Ole Serian anayeongoza oparesheni dhidi ya waasi hao katika msitu wa Boni.

Ole Serian anasema vituo hivyo vitafunguliwa katika maeneo ya Bothei Pandanguo na Mananguo. Anasema wanazuilia washukiwa kadhaa walionaswa katika maeneo ya Lamu, Garsen, Boni na Baragoni kufuatia oparesheni hiyo.

Ole Serian anasema ili kuleta utulivu serikali imetuma naibu kamishna wa kaunti hiyo pamoja na wasaidizi 12 katika maeneo ya Ijara, Hulugho, Lamu mashariki na Lamu.

No comments: