Wednesday, 16 March 2016

CHUO KIKUU CHA KIBABII CHAFUNGWA.


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Kibabii.

By Lena Juliet.

Chuo kikuu cha Kibabii kimefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuandamana na kusababisha uharibifu wa mali.

Wanafunzi hao wanasemekana kughadhabishwa na hatua ya usimamizi wa chuo kumuunga mkono mmoja wa wagombeaji kiti cha rais wao ambaye pia anafadhiliwa na serikali ya kaunti ya Bungoma na kumzuia mgombeaji mwengine kwa misingi ya kutomaliza karo.

Ghasia zilizuka kati ya makundi mawili ya wanafunzi kabla ya polisi kuitwa kuingilia kati. Katika vurumai hilo mtu mmoja alipigwa risasi kimakosa na amelazwa katika hospitali ya rufaa mjini Bungoma.

No comments: