![]() |
| Vinara wa Cord wakimpigia debe Willy Mtengo |
BEN KIRUI
Joto la kisisasa linazidi kupanda huku zikisalia siku za kuhesabu kabla ya wenyeji wa kaunti za Malindi na Kericho kuelekea kwenye debe kuamua mbivu na mbichi kwenye kinyang’anyiro cha useneta.
Joto la kisisasa linazidi kupanda huku zikisalia siku za kuhesabu kabla ya wenyeji wa kaunti za Malindi na Kericho kuelekea kwenye debe kuamua mbivu na mbichi kwenye kinyang’anyiro cha useneta.
Muungano wa CORD umepiga kambi Malindi kumpigia debe Willy Mtengo atakayepeperusha bendera
ya chama cha ODM.
Vinara wa
CORD Raila Odinga na Kalonzo Musyoka waliongoza kampeni hizo katika eneo la Mwachiche
kaunti ya Malindi ambapo waliwarai wenyeji kumchagua Willy Mtengo.
Wakaazi wa
Kaunti za Malindi na Kericho wataenda debeni siku ya jumatatu kwa uchaguzi
mdogo wa useneta kuziba pengo zilizoacha wazi na Dan Kazungu Kambi na Charles
Keter mtawalia ambao waliteuliwa kuwa mawaziri.
Huku hayo yakiarifiwa mgombeaji wa
chama cha Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Malindi Philip Charo, amepigwa jeki baada
ya wagombeaji wawili kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho ili kumuunga mkono.
Wagombeaji hao, Peter Ponda wa Chama
Cha Uzalendo na Fuad Kombe wa Federal Party of Kenya, wamesema wameamua
kujiondoa ili kumuunga mkono mgombeaji huyo wa Jubilee.

1 comment:
Itakuwa vigumu sana kwa Charo ikizingatiwa kwamba Malindi ndio ngome ya Cord
Post a Comment