Wednesday, 20 April 2016

BENKI YA CHASE KUFUNGULIWA WIKI IJAYO


Benki ya Chase ilifungwa na kuwekwa chini ya urasimu
Ben Kirui

Afueni kwa wateja wa benki ya chase baada ya benki kuu ya Kenya kutangaza kwamba wateja hao wataweza kupokea huduma za benki hiyo siku ya jumatano wiki ijayo.

Benki hiyo iliyowekwa chini ya urasimu majuma mawili yaliyopita itafunguliwa kufuatia makubaliano baina ya benki ya KCB na washika dau wengine kuchukua hisa za benki zake.

Gavana wa benki kuu ya Kenya Dkt Patrick Njoroge ametangaza kuwa matawi yote 62 ya benki hiyo, yatafunguliwa tena ifikapo tarehe 27 mwezi huu.

Hata hivyo wateja wataruhusiwa kutoa hadi shilingi milioni moja huku wanaotaka kutoa zaidi ya milioni moja watasubiri hadi mchakato wa kuweka mkakati wa kupata fedha hizo utakapokamilika.

No comments: