Wednesday, 20 April 2016

WASHUKIWA WANANE WA UJAMBAZI WAUAWA MUKURU.

Washukiwa hao wamekuwa miongoni mwa genge ambalo limekuwa likihangaisha wakaazi
Ben Kirui

Washukiwa wanane wa ujambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi katika mtaa wa Mukuru kwa Reuben.

Katika kisa hicho cha usiku wa kuamkia leo, bunduki nne, visu viwili, simu 12 za rununu ambazo zinaaminika kuibwa pamoja na sare rasmi ya polisi zilinaswa kutoka kwa majambazi hao.


Kulingana na kamanda wa polisi wa eneo la viwandani Nehemiah Langat, washukiwa hao ni miongoni mwa genge ambalo limekuwa likihangaisha wakaazi kwa muda.

No comments: