![]() |
| Rais Uhuru Kenyatta |
Ben Kirui
Rais Uhuru
Kenyatta amemtaka kinara wa Cord Raila Odinga kuacha kuchafulia taifa hili jina
wakati wowote anapozuru nchi za ngambo.
Hii ni
kufuatia matamshi ya Raila kwamba ICC ilikosea kwa kufutilia mbali kesi
iliyokuwa ikikabili wakenya sita katika mahakama ya ICC katika mahojiano na kituo
kimoja cha televisheni nchini Ufaransa.
Akizungumza wakati
wa ziara yake katika kaunti ya Nyandarua, Rais alionekana kukerwa na matamshi
ya Raila akisema ikiwa mahakama ya ICC iliridhika kuwa naibu rais William Ruto
na Joshua Sang’ hawakuwa na kesi ya kujibu sio sawa kwa Raila kuendelea
kuikosoa mahakama hiyo kwa uamuzi wake.
Kwa upande mwingine
naibu wake William Ruto alisema hatua ya ICC kutupilia mbali kesi iliyokuwa
ikimkabili imewakera mahasimu wao kisiasa ambao walidhania wangepata fursa ya
kuiongoza taifa hili ikiwa mambo yangeenda mrama

No comments:
Post a Comment