Wednesday, 25 May 2016

EACC YAFICHUA UFUJAJI WA FEDHA NA WAKUU WA SHULE



Waziri wa Elimu Dkt Fred Matiang'i



Na Liz Wanjiru

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imetoa ripoti inayoonyesha kuwa fedha za kufadhili elimu bila malipo zinafujwa na wakuu wa shule.

Akiongea baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo inayoonyesha ufujaji wa fedha na EACC, waziri wa Elimu Dkt Fred Matian’gi amesema kuwa  ufisadi huo umechangia kudunisha elimu ya bure nchini huku akipendekeza mabadiliko kufanywa ili kurekebisha hali.

Kulingana na ripoti hiyo fedha hizo zimepotea wakati ambapo zabuni hutolewa kwa njia isiyo halali.

No comments: