Sunday, 22 May 2016
PIGO KWA ODM BAADA YA MBUNGE MMOJA KUKIGURA CHAMA HICHO
Ben Kirui
Chama cha ODM kimepata pigo baada ya mbunge mmoja kuhamia mrengo wa Jubiee akilaumu chama hicho kwa kujihusisha na ghasia na ukiukaji wa sheria.
Akizungumza wakati wa ziara ya mwisho ya rais Uhuru Kenyatta eneo la kaskazini mashariki katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Garissa, mbunge wa Ijara, Ahmed Ibrahim Abbass, amemlaumu kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kwa kuwazungusha wafuasi wa chama hicho bila rekodi yoyote ya maendeleo.
Mbunge huyo amekuwa akikosoa uongozi mkuu wa chama hicho, hasa kutokana na kuanguka kwa Mswada wa Okoa Kenya akilaumu Kamati Tekelezi ya Muungano huo kwa kazi duni, ambayo ilipelekea kuanguka kwake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment