![]() |
| Gavana wa Bomet Isaac Ruto |
Ben Kirui
Gavana wa
Bomet Isaac Ruto, amepuuzilia mbali wakosoaji wake na kusisitiza kwamba angali
ndani ya Jubilee na kusema hajawahi kuondoka na hataondoka kwenye muungano huo.
Akizungumza
na wanahabari nyumbani kwake, Ruto amesema tofauti zinazokisiwa kuwepo kati
yake na Naibu Rais William Ruto ni sintofahamu iliyoundwa na wabunge wa eneo
hilo ambao wameamua kuendeleza ajenda zao bila kumshirikisha.
Gavana Ruto
amekuwa akionekana kukosoa serikali ya Jubilee huku kwa mara nyingi akitofautiana
na Naibu Rais William Ruto hadharani.

No comments:
Post a Comment