Na Editer Wakesho
Waziri
wa maswala ya usalama wa ndani Joseph Nkaissery amesema polisi
watawatia pingu vinara wa CORD, endapo watakwenda kinyume cha
sheria.
Nkaissery amesema serikali
imeipa CORD muda mwingi wa kujieleza kwa mapendekezo yao, walakini sasa
haitaruhusu yeyote kujihusisha na ukiukaji wowote wa kisheria na vitisho
vinavyoelekezwa kwa serikali.
Aidha
Nkaissery amesema Raila Odinga, Moses Wetangula, Kalonzo Musyoka na seneta wa
Siaya James Orengo na mwenzake wa Machakos Johstone Muthama watashikwa endapo
watavunja sheria akiongezea kuwa hawataruhusiwa kuandaa mkutano wowote
katika bustani ya Uhuru.
Pia
alisema kuwa ni rais pekee aliye na mamlaka ya kuongoza sherehe
sampuli ya Madaraka wala sio yeyote mwingine..
Matamshi
yake Nkaissery yanakuja huku mvutano ungali ukiendelea kutokota kuhusu ni nani
atakayeruhusiwa kuandaa mkutano katika bustani ya Uhuru kati ya CORD na kanisa
la Prayers Beyond Boundaries linalodai kwamba lilikuwa la kwanza kutwaa ruhusa
ya kuitumia.

No comments:
Post a Comment