![]() |
| Nyota wa PSG Marco Verratti. |
Mwangi K.Githinji.
Manchester United
wameanza kumtupia jicho kiungo wa Paris Saint-Germain Marco Verratti .
Inakisiwa kuwa United
wanatayarisha dau la pauni yuro milioni 79 ili waweze kumshawishi ajiunge nao.
Verratti mwenye umri wa
miaka 23 ameichezea PSG mara 157 tangia alipocheza mechi yake ya kwanza mnamo
mwaka wa 2012 akiwa bado chipukizi.
Inaaminika kuwa kocha Jose
Mourinho ni shabiki mkubwa wa Muitalia huyo ambapo yupo makini kuona kuwa
anakipiga na klabu chake msimu ujao.
Iwapo watamtwaa Verratti, watamlipa donge nono la yuro milioni
6.7 kwa msimu huku ikielezewa kuwa mchezaji Zlatan Ibrahimovic anataka wahamie
united pamoja.

No comments:
Post a Comment