Tuesday, 14 June 2016

KOCHA WA BRAZIL APIGWA KALAMU.










Kocha wa Brazil Dunga.
Mwangi K. Githinji.

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Dunga amefutwa kazi kufuatia kuondolewa kwa timu hiyo kutoka kwa michuano ya Copa America.
Shirikisho linalosimamia soka la nchini Brazil  (CBF) limedhibitisha kuwa mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 52 ameondoka ,ambaye aliifunza timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.
Brazil waliondolewa kutoka kwa dimba la Copa la mwaka huu kwa mara ya kwanza tangia mwaka wa 1987  katika awamu ya makundi baada ya kupoteza 1-0 kwa Peru siku ya Jumapili.
Hii ni licha yao kuanza michezo hiyo vizuri kwa kuandikisha sare moja na kisha kuifunga Hait mabao 7-0.

No comments: