![]() |
| Viongozi wa Cord James Orengo na Johnstone Muthama wakihutubia wanahabari awali |
Ben Kirui
Muungano wa Cord umefutilia mbali
maandamano yaliyokuwa yameratibiwa kufanyika katikati ya jiji hii leo.
Viongozi wa
cord wamesema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya wenzao wa jubilee kuonyesha
nia njema katika mchakato wa mazungumzo kutafuta suluhu wa utata unaokabili
tume ya uchaguzi na maeneo mipaka nchini IEBC.
Hata hivyo Wanakamati
simamizi katika muungano wa Cord James Orengo na Esely Simiyu wanaonya kwamba
maandamano hayo yatarejelewa jumatatu na alhamisi ijayo endapo mazungumzo hayo
hayatazaa matunda.

No comments:
Post a Comment