Thursday, 9 June 2016

CARRICK ASAINI MKATABA WA MWAKA MOJA.



Mchezaji wa Manchester United Michael Carrick.







Mwangi K .Githinji.

Kiungo wa Manchester United Michael Carrick amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hicho.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 alipewa nyongeza ya mkataba huo na kocha mpya Jose Mourinho ambaye anaamini kuwa bado Carrick atakuwa nguzo muhimu anapojitayarisha kwa msimu mpya.Carrick alijiunga na United kutoka Tottenham mnamo mwaka wa 2006 na amefaulu kushinda mataji matano ya ligi na lile na klabu bingwa barani ulaya.Baada ya kusaini nyongeza hiyo kiungo huyo alieleza furaha yake kwa kupata nafasi ya kuichezea united huku akimtaja Jose kama kocha aliye na umahiri wa kushinda mataji kila aendapo.

No comments: