Friday, 17 June 2016

CONTE AMTUPIA JICHO MORATA.







Mchezaji Alvaro Morata.
Mwangi K. Githinji.

Chelsea wanawinda sahihi ya mchezaji wa Juventus Alvaro  Morata wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.

Morata amefunga mabao 27 katika mechi 93 alizochezea  Juve  tangia alipojiunga na miamba hao wa ligi kuu ya nchini Italia mnamo mwaka wa 2014 ,lakini kwa muda sasa ameendelea kuhusishwa na uhamisho wa kuvighuria vilabu kadhaa vinavyoshiriki ligi ya uingereza.

Inakisiwa kuwa donge nono la mshahara na pia ujio wa meneja mpya Antonio Conte huenda ukamshawishi kuenda Chelsea

Aidha mwakilishi wake alisafiri ugani Bernabeu ijumaa iliyopita ili kufanya mazungumzo na klabu cha Real Madrid.




No comments: