![]() |
| Nyota wa Dortmund mkhitaryan |
Mwangi K.Githinji.
Vilabu
vya Manchester United na Arsenal vimeingia katika vita mgao wa kula baada ya
ajenti wake kufichua kwamba staa wa Dortmund Henrikh Mkhitaryan angependelea
kuhamia United.
Miamba hao wa ujerumani
walidhibitisha usiku wa jana kuwa mchezaji huyo amekataa kusaini mkataba mpya
na klabu hicho huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa msimu wa
2017.
Itawalazimu Dortmund kufanya
uamuzi wa kumuuza ama kuendelea kumbakiza nyota huyo ama wampoteze baada ya kipindi
cha miezi 12, bila kulipwa ada yoyote.
Habari hizo ni pigo kwa Arsenal
ambao wanasaka sahihi ya nyota huyo Mkhitaryan
aliyekuwa anachezea klabu cha Shakhtar Donetsk hapo
awali.

No comments:
Post a Comment