Saturday, 18 June 2016

JONES NI MZURI KAMA TERRY-MOURINHO.



Beki wa Manchester United Phil Jones.
Mwangi K. Githinji.
Inaripotiwa kuwa Jose Mourinho ameeleza imani yake kwamba mlinzi wa Manchester United Phil Jones ana uwezo wa kufana sawai na kigogo wa Chelsea John Terry.
Jones alicheza mara 13 katika mashindano yote msimu jana jambo ambalo  lililopelekea wengi kutabiri kwamba huenda Jose akampiga bei.
Inakisiwa kuwa Mourinho alifanya kikao na mlinzi huyo ili kumhakikishia nafasi kwenye kikosi chake msimu ujao.
Mapema mwezi huu united walikamilisha usajili wa mlinzi Eric Bailly  kutoka Villarreal ambaye anatarajiwa  kuleta ushindani kikosini cha United.

No comments: